GET /api/v0.1/hansard/entries/1210814/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1210814,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1210814/?format=api",
"text_counter": 208,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sifuna",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13599,
"legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
"slug": "sifuna-edwin-watenya"
},
"content": "Bw. Spika, ninajua kwamba niko kwenye vitabu vyako vibaya na labda hunioni. Ninaomba tu mwongozo wako. Iwapo Seneta atasimama, azungumze na anitaje ama amtaje Seneta mwingine, mbona huwezi kumpa yule Seneta aliyetajwa, nafasi ya kujitetea, ili uamuzi wako nao ujumuishe maoni ya kila mtu? Ndugu yangu, Sen. Abdul Haji amezungumza na akataja mambo fulani kunihusu mimi kama Katibu Mkuu wa Chama. Hujanipa fursa nizungumzie madai ambayo ametoa dhidi yangu. Sio kulingana na mada ya barua ya mstahiki Kiongozi wa Walio Wachache. Madai aliyotamka dhidi yangu binafsi kama Katibu Mkuu wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM). Hilo ndilo lilikuwa linaniwasha hapa. Tumefika wakati ambao tunaona iwapo sheria ni msumeno wa kweli, ukate Sen. Sifuna na ukate wale wengine. Mimi ninahisi kana kwamba sisi wengine umetuweka pembeni na maoni yetu hayahitajiki kwenye mijadala katika Nyumba hii."
}