GET /api/v0.1/hansard/entries/1211053/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1211053,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211053/?format=api",
"text_counter": 50,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru Town East, UDA",
"speaker_title": "Hon. David Gikaria",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Mwanzo najua umesoma maombi haya. Sijajua utayaelekeza wapi. Nimesikia Mwenyekiti wa Kamati ya Afya akisema… Najua haya Maombi yanafaa kwenda katika Kamati ya Maombi ya Umma. Sisi kama Wajumbe, tunafaa tuangalie jambo hili kwa sababu Mwenyekiti wa Kamati ya Afya amesema Kamati ya Maombi ya Umma iwaalike wale ambao wanahusika. Pili, nakubaliana na vile Kiongozi wa Wengi Bungeni amesema. Kiongozi wa Wengi Bungeni alisema kuwa ni muhimu kuwatambua hao watoto mapema kupitia ule mtandao wa kisasa wa kibayometriki. Mheshimiwa amesema kuwa wanahitaji kutambuliwa mapema wakiwa shuleni na hata baada ya kutimiza miaka kumi na minane, wataendelea vile tulivyosema baada ya kupitisha Mjadala ama Sheria katika Bunge la Kumi na Mbili kuwa mtoto yeyote atakayetimia miaka kumi na minane ni lazima asajiliwe na NHIF . Ninakubaliana pia na Bw. Didmus Barasa kwamba ni muhimu mambo tunayoweka kwa Serikali yaweze kufanyiwa uchunguzi. Tukivumbua kitu fulani, kinafaa kufanyiwa uchunguzi fulani ndio tujue uzuri au ubaya wake kabla hatujaendelea. Ninaunga Mkono hii Dua. Asante sana Bw. Speaker."
}