GET /api/v0.1/hansard/entries/1211160/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1211160,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211160/?format=api",
    "text_counter": 157,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Migori County, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Serikali kuu haipati nafasi ya kufika mashinani kujua shida za wananchi. Kwa hivyo, hizi pesa zinatusaidia. Kusema kweli, tunatumia hiki kiti ili kutetea mambo mengine lakini bila NG- CDF na NGAAF, hakuna maana ya kuwa Mbunge kwa sababu wananchi wanaangalia hizi pesa tunazozipata kupitia hiki kiti. Ingekuwa juhudi yangu binafsi ningeamrisha leo hii hizi pesa ziwekwe kwenye Katiba bila kuwauliza wananchi kwa sababu wananchi tunaowaakilisha wanatusukuma kila siku wakituuliza mbona inasemekana hivyo. Kusema kweli, hii si haki. Hizi pesa ziwekwe kwenye Katiba ndiyo wanachi wapate haki yao."
}