GET /api/v0.1/hansard/entries/1211161/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1211161,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211161/?format=api",
"text_counter": 158,
"type": "speech",
"speaker_name": "Migori County, Independent",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Kwa upande wa kuongeza idadi ya wamama ndani ya hili Jumba, hii pia ni changamoto kubwa sana. Hadi sasa tuna upungufu mkubwa sana. Hata ndugu zetu ambao ni Wabunge wenzetu, wanakubaliana na sisi kuwa idadi yetu iko chini. Hata sasa, sisi ambao ni waakilishi wa wamama tunaambiwa ya kuwa uchaguzi ujao utakuwa mwisho wa kiti hiki. Hapo tayari imeleta baridi kwa wananchi na wamama. Sasa hii wanatubabaisha wakituambia baada ya uchaguzi ujao kiti cha wamama hakitakuwepo tena na hatuna idadi ya kutosha, tukifikia uchaguzi mpya na hiki kiti kifanyiwe uchaguzi wa mwisho huenda kukakosekana hata mama mmoja kwenye hili Jumba. Tunapaswa kupitisha Hoja hii haraka sana bila kurudi kwa wananchi. Kuna yale ambayo yatahitaji turudi kwa wananchi kwa njia ya referendum ili watuambie kama wanakubali maneno tunayoyazungumzia ndani ya hili Jumba. Kuhusu NG-CDF, NGAAF na kuongeza idadi ya wamama kwenye hili Jumba, Wakenya wanakubaliana na sisi kwamba ni muhimu na inapaswa kuharakishwa. Kuhusu waliochaguliwa kama c abinet secretaries kuja ndani ya hili Jumba, sijui kama kutakuwa na haja ya kamati. Kwa sababu kama wakikuja hapa kujibu maswali, basi hakuna haja ya kamati kuketi chini na kutumia hela ya wananchi kumwita mkubwa mwingine aelezee vile pesa zinatumika katika Idara. Maoni yangu ni kama tunafanya kazi moja kwa mikono miwili. Hakuna haja mtu mwingine akuje hapa kuzungumza na kwenye kamati mtu mwingine anazungumza maneno mengine. Hii haina maana kabisa. Kama tunataka wakuje katika hili Jumba, basi wachaguliwe kati yetu tulio hapa ndio wanaamka kutetea jambo linalozungumziwa kwa haraka ndio tupate majibu na tuwachane na mambo ya kamati ama tuendelee na kamati ili wakuje tuwaulize maswali. Ukiangalia idadi ya Wabunge walio ndani ya hili Jumba, tunaelekea mia 400. Ni wakati mgani mmoja wetu atapata nafasi ya kuzungumza na huyo c abinet secretary akija hapa? Kwa sababu kuja kwake hapa itakuwa muda mfupi, huenda ni dakika ishirini ama thelathini, ni nafasi gani kila mmoja atapata ili azungumze yale ambayo angependa kumuuliza? Lakini kwenye kikao cha kamati kama uko na neno umekubaliwa kufika pale maanake kuna Wabunge 15 na ikienda sana 20."
}