GET /api/v0.1/hansard/entries/1211165/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1211165,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211165/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Migori County, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Nikiangalia desturi ya hili Jumba, huenda ni waheshimiwa wawili ama watatu watapata nafasi ya kuzungumza. Sisi kama waakilishi wa kina mama au wachache ndani ya Bunge hatutapata nafasi ya kuzungumza na yule Waziri atakapokuja. Kwa hayo machache, ningependa kusema kuwa lililo la muhimu sana na lenye dharura ni swala la NG-CDF na NGAAF lipitishwe bila kupelekwa kwenye kura ya maoni. La pili ni swala la uwakilishi wa akina mama katika Bunge lipitishwe bila hata kupelekwa kwenye kura ya maoni. Mengine yanahitaji kina Wanjiku na Atieno wajisemee iwapo wanapenda ama hawapendi hiki kifanyike. Kwa hayo machache, nashukuru Naibu Spika wa Muda."
}