GET /api/v0.1/hansard/entries/1211169/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1211169,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211169/?format=api",
    "text_counter": 166,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Emurua Dikirr, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Johana Kipyegon",
    "speaker": null,
    "content": "ambayo ilitumwa na Rais wa Jamhuri ya Kenya hapa Bungeni ili tujaribu kuangazia na kuangalia tutakavyo endelea. Watu wengi wanauliza iwapo sheria hubuniwa na Bunge. Ni kweli kuwa ubunifu wa sheria ama waliopewa jukumu hilo na Katiba ya nchi ni sisi Wabunge. Lazima tuzitambue zile sehemu tatu za Serikali ambazo ni Bunge, Executive na Mahakama. Wakati mwingine tukibuni sheria mahakama inaweza ipinga hiyo sheria kwa madai ya kuwa kinyume na Katiba na kutoa mwelekezo. Wakati mwingine, tunazitumia zile precedences za mahakama kama sheria. Hata hivyo, ijapokuwa sheria inasema kuwa sisi ndio watunzi wa sheria, kuna sehemu za Serikali ambazo zimepewa jukumu la kubuni sheria. Wakati mwingine, Executive hubuni sheria zao zinazopitishwa hapa Bungeni. Ninaamini kuwa Rais kuwaandikia Wabunge kuwaeleza mtazamo wake si kosa. Hii ndio fikira langu Jambo la muhimu ambalo Rais amezungumzia haswa kuhusu kazi tunayofanya Bungeni ni kupendekeza mawaziri waje kwenye Bunge. Aliomba Bunge ipitishe hilo pendekezo kupitia kwa Kauni za Kudumu. Tutazibadilisha ili kuhakikisha kuwa wale mawaziri ambao tunataka kuuliza maswali waje hapa wayajibu. Lakini ninaamini kuwa suluhu ya kudumu ni kuangalia iwapo tunaweza badilisha Katiba ya Kenya, ijapokuwa tunajua uongozi wetu ni p residential system . Nia ya Rais kuwatuma mawaziri hapa ni kuhakikisha kuwa mahali tulikuwa tunafanya ukaguzi wa mawaziri haikufanyika vizuri. Sasa, pendekezo hili litahakikisha kuwa ukaguzi wa mawaziri unafanywa vizuri kwa sababu utaonyeshwa kwa uwazi. Ni maoni yangu kuwa tunaweza kuamua kuibadili sheria kwa kuwa hatukuandikiwa sheria bali tuliandika sisi wenyewe lengo likiwa kurahisisha maisha ya mwananchi. Haikuandikwa iwe kitu cha kutudhuru. Tukibuni sheria na baadaye isitimize lengo lake ni jukumu letu kama wananchi tukipiga kura ya maoni tuhakikishe kuwa tutarekebisha pale ambapo hapastahili kuwa. Tukiona kuwa presidential system haifanyi kazi, tunaweza ibadilisha tuwe na ile inaitwa hybrid, yaani ule mchanganyiko maalum. Kuna Rais anayechaguliwa na raia na mawaziri wanaochaguliwa kutoka kwa Wabunge ili wafanye kazi ya uwaziri wakiwa kwenye Bunge. Ninaamini Rais alitaka tuzoee kuleta mawaziri Bungeni. Ninaunga mkono. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}