GET /api/v0.1/hansard/entries/1211170/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1211170,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211170/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Emurua Dikirr, UDA",
"speaker_title": "Hon. Johana Kipyegon",
"speaker": null,
"content": "Jambo la pili ambalo Rais amezungumzia sana ni swali la t wo third gender rule . Waandishi wa Katiba ya Kenya walishindwa kupata suluhisho. Inakuwaje kuwa waliopewa jukumu la kuandika Katiba walizunguka nchi nzima na wakaenda Naivasha kuandika sheria lakini dakika ya mwisho wakaweka kipengele cha kulipatia Bunge hilo jukumu? Ni kwa sababu ni kitu kigumu sana. Bunge zote kuanzia Bunge la 11, Bunge la 12 na Bunge la 13 hazikuweza kushughulikia swala la t wo third gender rule . Kama tunataka kuwasaidia wanawake ni lazima tubuni sheria inayosema kuwa katika kila uteuzi, asilimia hamsini kwa mia iwe ya kila jinsia. Hiyo itawezekena kukiwa na uwezo ya kuteua watu wala si kuchaguliwa. Ukipewa hiyo nafasi, unaweza amua kulingana na sheria kuteuwa wanawake kwa wanaume. Katika uchaguzi, ni raia anayeamua bila kujali iwapo wewe ni mwanamme au mwanamke. Anakuchagua kulingana na anayohisi iwapo unastahili kuwa kiongozi wake. Katiba inasema kuwa uchaguzi ni kupitia universal suffrage. Sijui kutafsiri kwa Kiswahili. Kiswahili kilikuja kwa miguu kikatupata barabarani tukienda, kwa hivyo kuna vitu hatufahamu. Hiyo universal suffrage inaruhusu mwananchi kumchagua mtu yeyote hata kama ni kiwete au mwanaume. Uchaguzi unategemea mtu mwenyewe. Tukitaka suluhisho la kudumu kwenye sheria itabidi tuirekebishe baadala ya kuchagua ili iwe hamsini kwa hamsini. Jambo la mwisho ni la NG-CDF. Namshukuru Rais kwa kuunga mkono NG-CDF. Mtu yeyote ambaye amewahi kuwa mbunge wa Kenya ama amewahi kutafuta kiti cha kuwa mbunge hawezi kubali NG-CDF itolewe. Wale watoto ambao wamesoma kwa kutumia NG-CDF huko vijijini kama wamefika chuo kikuu ama wamemaliza, na wale wako shule ya upili hawawezi kukubali itolewe. NG-CDF ni kama ile kitu inaleta usawa mahali ambapo serikali za kaunti na Serikali ya Kitaifa zimeshindwa kufanya na kufikia. Hizi ni pesa ambazo zinaenda mpaka mahali Rais ama gavana hawawezi kufikia. Rais alikuwa Mjumbe wakati fulani. Ameelewa yakwamba NG-CDF iko na maana. Sisi kama Wajumbe tutasaidiana tuhakikishe kwamba tumeiweka kwa Katiba ya Kenya, ndio isije ikawasumbua watoto wetu ambao watakuwa Wajumbe baadaye."
}