GET /api/v0.1/hansard/entries/1211494/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1211494,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211494/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "ningependa kupongeza hatua ya kwamba tuhifadhi fedha hizo ndani ya Katiba yetu ili tuweze kusaidia jamii kule mashinani. Mpaka sasa, wengi wa watoto wetu wako nyumbani kwa sababu kuna mtu aliamka siku moja asubuhi akaona kuwa watoto wanaopewa hizi pesa za ufadhili hawafai. Kwa hivyo, sharti tuweke migao hiyo kwenye Katiba. Hata hivyo, hiyo ni sheria na mimi naunga mkono kuwekwa kwa mgao huo ndani ya sheria ili uweze kufikia wananchi kule chini. Jambo lingine ambalo limezungumziwa katika mjadala wa leo ni kuhusu kiongozi wa upinzani. Inasikitisha sana kwa sababu siku zote wenzetu wakisimama kuongea utasikia wako kule Kamukunji ama Mavoko lakini huwezi kuwasikia kanisani. Ningependa kusema kuwa ni lazima tuweke heshima na tusikumbushane kule tumetoka. Ni nani alimwibia mwenzake? Ni nani alipita na ni nani hakupita? Hii ni kwa sababu kama tunataka kujenga taifa, basi ni lazima tuwe na mwafaka wa kuheshimu kwa viongozi wote. Siwezi kukaa katika Bunge hili nikiona kiongozi wangu wa chama akidhalilishwa. Hata kama hawataji majina huwa naelewa wanaenda wapi. Kwa hivyo, ni lazima tuheshimiane. Tumheshimu pia kwa sababu alikuwa kiongozi ambaye alipigania taifa hili na aliweza kutuletea Katiba hii ambayo tunaifurahia leo kama akina mama 47 ndani ya Bunge hili. Mhe. Raila aliweza kuipigania Katiba hii ya 2010 na leo hii tunazungumzia kuhusu thuluthi mbili ya wanawake ndani ya Bunge kwa sababu yake. Ningependa apewe heshima na tuheshimu viongozi wetu wote. Najua pengine wengine wako kule kwenye chai na wanatazama kwenye televisheni. Labda wameweza kumgusa gusa hapa na pale lakini ningependa kuwaambia kuwa mimi kama mama Kaunti Mombasa, siwezi kukubali hilo. Tumheshimu Baba Raila Amolo Odinga kama tunavyostahili kuheshimu viongozi wengine. Ningependa pia kusema hili: ukiangalia Serikali iliyopo, inasikitisha sana kwa sababu leo mijadala ambayo imeletwa hapa ni juu ya vyeo…"
}