GET /api/v0.1/hansard/entries/1211498/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1211498,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211498/?format=api",
"text_counter": 208,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, ndugu yangu Mhe. Ndindi kwa kuweka hilo wazi. Nikiendelea, ningependa kusema kuwa mijadala ambayo imeletwa Bungeni leo ni juu ya vyeo. Kwa mfano, kuna Hoja kuhusu kupewa cheo cha Parliamentary Service Commission (PSC) kwake Mhe. Muthama, ambaye tunampenda sana. Tunamtakia kila la heri lakini awe na jicho la tatu kuangalia pande zote kama alivyosema Kiongozi wa Wachache Bungeni. Ahakikishe nafasi za kazi zinapewa pande zote bila kuzingatia kabila, chama wala rangi. Ninampongeza sana kwa hilo. Lakini, masikitiko yangu makubwa ni kuwa Wakenya wanakufa njaa. Ninawakumbuka ndugu zetu wa Mkoa wa Kaskazini Mashariki, Tana River na wengineo. Ukiangalia kila sehemu, watu wanakufaa njaa. Wakenya wanahangaika. Wanyama wanakufa. Kama Wabunge, ningependa tuweze kupanua akili zetu kwa upana zaidi na kuhakikisha kuwa wale waliotupigia kura wakatuwezesha tuje Bungeni tunawapa kipaumbele. Njaa imekuwa baa la kustaajabisha sana katika hili taifa lakini tumelifungia hilo tatizo macho. Leo hii, twazungumza mambo ya vyeo na mengineyo. Tumesahau mamilioni ya Wakenya. Leo hii, hawajui wataweka nini mdomoni. Wanatafuta hata maji na ndiyo maana mimi nakubaliana na huu mjadala unaosema tuwalete mawaziri hapa Bungeni ili waweze kuwajibika. Leo tunataka kuwauliza: wamepewa nafasi ya kuwa mawaziri, kwa mfano, Waziri wa Kilimo au Waziri wa Maji; je, wamepanga mikakati gani? Akili yao wameipanua vipi ili janga hili la njaa waweze kupigana nalo kuhakikisha kuwa kule Turkana, Kaskazini Mashariki, Mwakirunge, na Mombasa watu wanapata chakula? Hatuwezi tukakaa siku zote, miaka nenda, miaka rudi tukisumbuliwa na hili tatizo. Njaa imekuwa kitu cha kurejelewa! The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}