GET /api/v0.1/hansard/entries/1211499/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1211499,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211499/?format=api",
    "text_counter": 209,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Dubai ni nchi jangwa lakini leo hii ni kijani kibichi kila sehemu. Jua linachoma mpaka katikati ya utosi, lakini leo hii wanatoa matunda na mboga nzuri na safi kwa sababu wamepata viongozi wenye msukumo na wanaowafikiria wananchi. Dubai iliyokuwa jangwa, leo inazalisha chakula kingi zaidi. Kwa hayo, ningependa kueleza Waziri wa Kilimo kuwa wakulima wanalalamika kuwa mbolea iliyotolewa bure inauzwa Ksh3,500. Tunataka Wakenya wapate chakula lakini maji tunayaongeza ushuru, mbolea zinauzwa, na shamba nazo zimekuwa adimu. Tutawezaje kubadilisha maisha ya Wakenya ikiwa tunawaweka katika hali ngumu Zaidi, hasa wakulima? Wabunge wenzangu, ningeomba tuweke historia ya kubadili maisha ya Wakenya katika hili Bunge la Kumi na Tatu. Tunafaa tufuate Katiba. Wabunge wa jinsia ya kike ni wengi humu Bungeni. Sitawataja majina lakini inasikitisha sana kuwa Mbunge mmoja hapa amesema katika mkutano mahali kuwa, kina mama wanatakia nini kujaza Bunge. Amesema eti watakuja kuwa"
}