GET /api/v0.1/hansard/entries/1211501/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1211501,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211501/?format=api",
    "text_counter": 211,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "na “slay queens”. Ningependa kumwambia mahali yuko kuwa, pengine akimleta mkewe hapa tutaweza kumbandika hilo jina “slay queen”. Hatuwapei heshima waheshimiwa wa jinsia ya kike humu Bungeni. Hatujakuja hapa kwa matani na kutafutana na watu bali kuwatafutia Wakenya haki zao. Tuko hapa kuangalia vile tunaweza kuboresha maisha ya wananchi na hadhi ya mama katika hili taifa ili aweze kuheshimika. Siyo popote utakapomuona mwanamke unafikiria tu mambo ya ngono. Hapana! Tunataka heshima kwa akina mama. Nikimalizia, katika yale yamezungumzwa leo kuna jambo kuhusu IEBC. Hatuwezi kusema kila siku tutatunga sheria ili kumwezesha kiongozi wa upinzani… IEBC inaweza kupeleka taifa hili katika vita vya kila siku! Ndiyo maana ningependa kuwaambia wenzetu hivi: mtakuwa mwatudhalilisha na kutuita majina yote kama vile the Kamkunjis na Mavokos, lakini it ends with IEBC. Sisi tunataka usawa. Nikiumwa leo na ucheke, jua kesho utaumwa pia. Kwa hivyo, ikiwezekana waweke usawa katika tume ya IEBC ili iweze kuhudhumia Wakenya kwa usawa na kila mmoja apate haki yake. Leo mama Zamzam nikianguka, nijue nimeanguka kwa haki. Dadangu Nyakaira akianguka, ajue pia ameanguka kwa haki. Mambo ya kufanya filfinyange kisha Kenya iingie kwenye mtihani hatuwezi kukubali. Ninaona muda wangu umeisha lakini kama mama Mombasa, ninaunga mkono mjadala huu wa leo wa kuweka ofisi hii rasmi ya kiongozi wa upinzani na kuweka two-thirds gender"
}