GET /api/v0.1/hansard/entries/1211945/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1211945,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211945/?format=api",
"text_counter": 28,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, jana tuliambiwa na Spika - na wewe Naibu Spika ukiwepo ndani ya Seneti – kwamba, hivi leo, taratibu ambayo ilichukuliwa na upande wa Walio Wachache itaweza kuletwa hapa kama Ujumbe kulingana na yale mageuzi ambayo Upande wa Walio Wachache, waliyaleta ndani ya Seneti. Bw. Naibu Spika, ninaomba kusikizwa kwa kimya. Jana tulipokuwa hapa, Spika alituahidi ya kwamba, leo atatoa Uwasilisho kutokana na malalamishi yaliyotolewa na Upande wa Walio Wachache. Bw. Naibu Spika, wewe ulikuwa hapa wakati ahadi hiyo ilitolewa. Uwasilisho wenyewe ulitakiwa kutoa mwongozo kutokana na mageuzi yaliyoletwa hapa Bungeni na Upande wa Walio Wachache. Katibu amesimama na kusoma shughuli ya Uwasilisho kutoka kwa Spika katika Ratiba ya Bunge. Ni kwa sababu tulipaswa kusikia Uwasilisho wa Spika. Hata hivyo, nimeona hakuna Uwasilisho wowote na umeendelea hadi shughuli ya nne. Umekosa kuleta yale mawasiliano. Bw. Naibu Spika, ninaomba kujua kuhusu yale mawasiliano ambayo tulikuwa tumewasilisha kwako na ukaahidi kuleta haba Bungeni leo. Hivi sasa, umeenda katika kipengele cha nne. Upande wa walio wachache hawana Kiranja wala Naibu wa Kiranja. Ulikuwa utufahamishe ili tujue iwapo uongozi upo, ndiposa tuweze kuendelea na Kanuni za Kudumu za Bunge la Seneti. Ni jambo la kusikitisha kwamba umepita shughuli ya tatu ya Uwasilisho wa Mwenyekiti. Tungependa kujua iwapo ulifanya uamuzi wowote. Unatakiwa kuleta Uwasilisho lakini sasa ninaona kuna kizungumkuti kinachoendelea. Tunataka kujua kwa nini hutaki kutupatia jawabu. Ni kizungumkuti gani kinachoendelea hapa, kiasi cha kwamba unanyima Upande wa Walio Wachache kuwa na viongozi wanaohitajika?"
}