GET /api/v0.1/hansard/entries/1212407/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1212407,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1212407/?format=api",
    "text_counter": 490,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, naunga mkono hayo yote yamesomwa hapa. Pia, ni aibu kubwa sana kwa yale yaliyotendeka siku ya leo katika Kenya kwa sababu walikuwa wanapiga kelele kama Mwenyekiti amekalia kiti. Tumeona yale waliokuwa wakisema kwa muda mrefu. Seneta alisema ile siku tutakuwa tukipitisha mambo ya Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) kutakuwa ni maandamano. Kwa hivyo, wametuonyesha aibu kubwa sana katika Kenya walipotoka nje. Hicho ni kitendo kimoja kibaya sana. Kwa hivyo, sisi watu wa Kenya Kwanza tutaendelea vizuri, tutasimamisha Kenya kwa kipindi ya miaka mitano. Pili, nikimalizia nasema kwamba yale wametenda yanaonyesha hawana aibu wala shukrani. Kile tunaomba ni mazuri kwa Serikali ya Kenya Kwanza ndio ituletee maji ya kilimo na suluhu kwa swala la janga la njaa na mengine mengi. Nyinyi hamna shukrani kwa wale watu waliowachagua. Jambo lingine ni maneno ambayo yalisemwa hapa na Sen. Sifuna kwamba alichaguliwa na kura nyingi kutuliko sisi wote. Hapa Kenya, hata kama ulichaguliwa kwa kura nyingi ama kidogo, sisi sote ni Maseneta. Mimi ni Sen. Munyi Mundigi kutoka Kaunti ya Embu."
}