GET /api/v0.1/hansard/entries/1212420/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1212420,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1212420/?format=api",
    "text_counter": 503,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Okenyuri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika kwa fursa hii. Ningependa pia kuunga mkono Hoja hii. Nashukuru viongozi wa chama kwa kunipa nafasi ya kutumikia wananchi katika Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali. Sisikitiki kuondolewa kutoka Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali kwa sababu nimejifunza mengi katika muda mfupi ambapo nimekuwa mwanakamati. Ninapojiunga na Kamati ya Biashara, Viwanda na Utalii, naahidi kutia bidii na kufanya kazi na Maseneta wenzangu. Nitawakilisha vijana na wananchi wote ambao wametutuma kufanya kazi katika Seneti. Ningependa kumkaribisha Seneta wa Bungoma, Sen. Wafula, ambaye atachukua nafasi yangu katika Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali. Tumefanya kazi nzuri na natumai pia ataendeleza kazi hiyo na kuwa kielelezo katika Seneti."
}