GET /api/v0.1/hansard/entries/1212465/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1212465,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1212465/?format=api",
    "text_counter": 548,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Ningependa kushukuru uteuzi wa Seneta mwenzangu aliyechaguliwa juzi kuhudumu katika Kamati ya Teknolojia. Wakati huu sasa, watu wanasonga katika mawimbi ya teknolojia na tuliwaahidi Wakenya kwamba shule za msingi, upili na vyuo vitaunganishwa na teknolojia. Tumeshuhudia mtandao wa pesa za bottoms-up, zile za Hustlers Fund unavyochunguza kupitia teknolojia. Sote tuliopewa nafasi kama mimi kuhudumu katika Kamati ya Ukulima, tutashughulikia masuala ya miwa, ngano na mifugo maeneo yaliyo na ukame ili kuhakikisha Wakenya wananufaika katika Serikali ya Kenya Kwanza. Bw. Naibu Spika, naunga mkono Hoja huu."
}