GET /api/v0.1/hansard/entries/1213465/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1213465,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1213465/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, kuna taarifa ambayo imeletwa kuhusu vile benki zetu zinavyowanyanyasa Wakenya kwa kuingia katika akaunti zetu na kutoa pesa kiholela. Ni vizuri haya mambo yaangaliwe kabisa. Unapata ya kwamba mtu katika akaunti yake, amewacha akiwa na kiasi flani cha pesa. Wakati anapoenda kutoa, pengine analipa hospitali ama anataka kulipa karo ya shule ya mtoto, anapata pesa tayari zimetolewa na zimetolewa kwa njia ambayo hafahamu na haelewi. Kamati yetu ya Fedha inapaswa iangalie haya mambo kwa kindani na wale ambao watapatikana wamekuwa wakiwalaghai Wakenya kwa njia ile, wachukuliwe hatua za kisheria na waweze kuchukuliwa hatua kali ili benki zetu zionekane zinafanya kazi ambazo zinapaswa kufanya, kulinda pesa zetu, na sio kuwalaghai na kuwaibia Wakenya ambao wana imani na wao. Kwa hivyo, naunga mkono taarifa iliyoletwa na Sen. Tabitha Mutinda. Kamati ambayo inajua inashughulikia mambo haya ikiongozwa na Seneta wa kutoka Kaunti ya Mandera, Sen. Ali Roba, atashughulikia mambo hayo kwa kindani na apeane taarifa ya kutosha. Asiogope mtu yeyote, benki zisiogopwe. Waangalie hayo mambo kwa kindani kwa sababu Wakenya wanadhulumiwa. Bw. Naibu Spika, jambo linalonishtua ni kwamba ukitoa pesa kidogo uliyo nayo, kwa benki, unasikia ya kwamba, kama sahii, Benki Kuu ya Kenya tayari wamerejesha. Wanasema wanarejesha yale malipo. Tayari unakatwa. Kuna wale ambao ni wakora tayari wameiba katika akaunti yako. Unashindwa, kwani unaishi katika nchi gani? Kama hautaibiwa na benki, pesa yako itachukuliwa na Benki Kuu ya Kenya. Mtu ya Kaunti ya Laikipia yule ambaye ana mifugo, ameuza mifugo amepeleka kwa benki. Kama mifugo haijaibiwa na wakora, unapata ataibiwa katika benki. Kama sio kwa benki, ni hii mambo ya kutoa ushuru wakati unatuma na hizi simu zetu. Unashindwa ukimbilie benki, hapana, ukimbilie simu, hapana, ukimbilie nani? Mimi ninaona kile ambacho kitakachofaa ni kukimbilia Kamati ambayo inahusika na tumtegemee Mwenyezi Mungu. Asante Bw. Naibu Spika."
}