GET /api/v0.1/hansard/entries/1213576/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1213576,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1213576/?format=api",
    "text_counter": 389,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, asante kwa nafasi hii. Ningependa kuunga mkono na kushukuru yale ambayo wakili, Sen. Mungatana, amewasilisha. Nimeona ya kwamaba ni kama mazoea ya viongozi wa Afrika kuwa na ugumu wa kutekeleza majukumu yao pasipo shinikizo za kisheria an zaidi ya hapo, kupewa adhabu kali. Tumekuwa katika Kamati mbali ambazo tumeona Kaunti zinakosa kujukumika kulipa mishahara, kodi, halmashauri za afya, watendakazi ama wanakandarasi. Haya yote yataweza tu kupata matibabu iwapo sheria ambayo ndungu yangu Seneta analeta. Itaweza kufanya kazi. Iwapo kaunti imepewa pesa za mishahara, yule anaye jukumika kulipa mishahara anapokosa kulipa ushuru, lazima apate kichapo cha mbwa mdomo juu. Pale ambapo wanakandarasi wamepewa kazi ya kufanya kwa mujibu wa muda fulani, wakose kufanya na wapate pesa, sheria iwepo vile wao pia wajukumike, kwa sababu wamepunja pesa ya mtozaji ushuru. Kwa hayo mengi, ningependa kuunga mkono Mswada wa wakili, Sen. Mungatana. Vile, vile katika majukumu ya Serikali, kulikuwa na asilimia 30 ya vijana wanawake na walemavu kupata kandarasi. Ukichunguza katika kaunti na Serikali, hayo yote yamesahaulika kwa sababu yale mapendekezo ambayo yako katika vitabu vya serikali, ni kama hekaya za abunwasi. Lakini iwapo sheria kama hii itapitishwa, na tupitishe katika kamati zetu na Bunge la Seneti, wale ambao wanahusika wasipofanya hivyo, vile watapata adhabu kali na wawe mfano kwa wengine ambao hudhani kwamba uongozi ni wa milele. Lazima wajue kwamba uongozi ni kama mapito na ni muhimu kutenda wema na kwenda zetu. Asante sana Bw. Spika wa muda."
}