GET /api/v0.1/hansard/entries/1214088/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1214088,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214088/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Molo, UDA",
"speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Kwa mara ya kwanza, nitajaribu kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili. Natumai kwamba sitafeli. Ningeanza kwa kumpa kongole Mbunge wa Githunguri, Mhe. Gathoni Wamuchomba, kwa sababu ya kuwafikiria wanafunzi wetu katika shule zetu. Wakati tunasema ya kwamba masomo ni ya bure, ni wazi tunasema uongo. Wakati tunasema ya kwamba masomo ya zile shule za kila siku ni bure, ama kwamba hakuna karo inalipwa huko, tunajua huo ni uongo. Tunaposema ya kwamba inawezekana kupeleka watoto katika shule za mabweni kwa wale wazazi wa hali ya chini, jibu ni kwamba huo pia ni uongo. Wakati nilikuwa kule mashinani Molo siku ya Jumapili, nilipatana na mama mmoja ambaye anauza sokoni. Mtoto wake alikuwa ameitwa shule ya upili ya Karoti Girls’ High School kule Kirinyaga. Yule mama alikuwa na risiti ya kuonyesha ya kwamba ameweza kulipa karo ya Ksh20,000 lakini, juu ya hiyo, alihitajika kulipa pesa zingine Ksh20,150 ya zile bidhaa ambazo zinahitajika pale shuleni ambazo alishurutishwa asinunue mahali pengine ila kule shuleni. Huyu mama ametia bidii. Kwa yule mama ambaye anauza nyanya sokoni kuweza kuweka Ksh20,000 ili aweze kumpeleka mtoto shuleni, ni juhudi kubwa sana. Aliponiambia kwamba amelipa karo, nikamuuliza kama alitafuta bursary . Aliniambia kwamba bursary haitaweza kulipa hayo mahitaji mengine. Ilibidi nitafute hela zangu kibinafsi ili niweze kumlipia, ili mtoto wake aweze kusoma. Ninafurahia ya kwamba huyo msichana ameanza maisha yake ya kidato cha kwanza katika shule ya Karoti kule Kirinyaga. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}