HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1214089,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214089/?format=api",
"text_counter": 134,
"type": "speech",
"speaker_name": "Molo, UDA",
"speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
"speaker": null,
"content": "Jambo hili lilinifanya nianze kufikiria: Hizi Ksh20,000 ambazo alikuwa anaitishwa ni za nini? Ukienda sokoni, shati ya shule ni Ksh350. Shati hilo hilo ukienda kulinunua kule shule ni Ksh800. Wanaongeza Ksh450, mara tatu ya zile pesa ambazo hiyo shati inagharimu huku nje. Vile vile, ile suruali ukinunua huku nje ni Ksh700, ilhali shule nyingi wanaziuza kwa Ksh1,500. Ukinunua sweta dukani ni Ksh750, lakini shule inauza Ksh1,500, mara mbili ya hiyo sweta ukinunua huko nje. Tai ya kawaida ukinunua sokoni ni Ksh150, ila ukienda kununua kule shule ni Ksh300. Tena wanasema ununue ile track suit . Ukiinunua dukani ni Ksh1,300, na ukienda kuinunua kule shule, wanauza kati ya Ksh2,000 na Ksh3,000. Godoro la kulalia, ukilinunua kwa duka ni Ksh1,800, ilhali mashule yetu yanaitisha wazazi pesa za kununua lile godoro, ambalo linakuwa hata ni dogo kuliko lile la Kshs1,800, na wanaitisha Ksh2,800. Nyingine ambayo linaitwa sweta ya kuruka, ambayo ya mtumba unaweza kupata na Ksh200, lakini kule shuleni wanaitisha Ksh2,500. Blanketi ukiinunua kwa soko ni Ksh500, lakini ukienda kuinunua shuleni, wanaitisha katikati ya Ksh700 na Ksh1,000. Vile vile, ile shuka ya kutandika kitandani, kwenye maduka ni Ksh600, ilhali shuleni ni Ksh1,000. Mto wa kulalia ukiununua kwa soko ni Ksh150, lakini shuleni wanaitisha kati ya Ksh300 na Ksh500. Na hakuna tofauti ya ule mto ambao uko kwenye soko na unaoitishwa na walimu wetu katika mashule. Ndoo ya kubebea maji au ya kusafisha nguo kwa soko ni Ksh150, ilhali shuleni ni kati ya Ksh300 na Ksh500. Zile soksi ukinunua dukani ni katikati ya Ksh50 na Ksh100. Waalimu wanaitisha katikati ya Ksh200 na Ksh500. Juu ya hayo, wanakuambia baada ya kulipa hizo pesa zote, kuwa lazima ulipe katikati ya Ksh500 na Ksh1,000 ili kuweka alama katika zile sare za shule. Kwa hivyo, ikiwa tunataka mtoto wa Mkenya yeyote aweze kwenda shuleni aweze kusoma na kufaulu katika Maisha, itabidi kuhakikisha ya kwamba tumeongeza pesa za ufadhili katika shule zetu. Lazima tupeane suluhu ya sare za shule na haya mambo mengine yote ambayo yanahitajika katika shule zetu. Njia rahisi kabisa ya kufanya hivyo ni kuhakikisha ya kwamba sare zote za shule za umma katika nchi yetu ya Kenya ziwe sawa. Shati iwe ni ya rangi nyeupe. Kama ni suruali, iwe rangi nyeusi au kijivu. Kuwe na kiwango kimoja kote nchini. Tukifanya hivyo, tutakuwa tumesaidia kupunguza gharama ya shule na, zaidi ya hayo, tutakuwa tumehakikisha ya kwamba yule fundi ambaye ako pale Mukinyai, Kapsinandet, Chandera, Arimi, na Kapsita, anaweza kushona hizo sare za shule na kusomesha watoto wake na kuweka chakula katika meza. Tumekuwa tukitengeneza sheria ambazo ni za kuhahikikisha ya kwamba wale mabwenyeye tu ndio wanaweza kunufaika kutokana na hizo sheria. Kwa mfano, hata ukiangalia shule zetu ambazo ziko mahali kwingine, unapoambiwa hii ndio barua ya kuingia shule, unaambiwa zile sare za shule lazima ununue kwa maduka fulani. Siyo ya kwamba hayo maduka mengine hayana hizo sare; sio ya kwamba bei yao ni nzuri kuliko maduka mengine; lakini unashurutishwa hivyo kwa sababu kuna lile agano ambalo mwalimu amefanya na hilo duka maalum. Na unapata hayo maduka hayana kitu kubwa. Ni vile tu hao ni mabwanyenye, na wameweza kujikimu kimaisha. Ndio unapata wale ambao wako na hela katika nchi hii wanaendelea kupata zaidi. Wale amabo hawana, wanaendelea kukosa zaidi. Kwa hivyo, kuna wale ambao waliongea hapa awali wakasema basi kama sare zote za shule zitakuwa sawa, pengine hakutakuwa na maridadi. Na mimi nakumbuka ya kwamba yule ambaye alikuwa Daktari Matiang’i alikuwa na makosa mengi sana. Alifanya mambo mengi mabaya. Lakini kama kuna jambo moja alifanya nzuri, ni kusema ya kwamba basi zote za shule katika Kenya ziwe na rangi moja. Unamkumbuka yule ambaye alikuwa Waziri wetu wa Uchukuzi – na apumzike kwa amani Marehemu Mheshimiwa Michuki - alisema kwamba wale ambao ni madereva na makanga wa magari yetu wavae sare moja - wengine zile za rangi ya maroon na wale wengine wavae rangi ya blue kwa madereva. Ukienda kwenye eneo lolote la uchukuzi katika nchi yetu, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}