GET /api/v0.1/hansard/entries/1214090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1214090,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214090/?format=api",
    "text_counter": 135,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Molo, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
    "speaker": null,
    "content": "utaweza kujua huyu ni dereva na huyu ni makanga. Na pia, kwa kununua zile sare, unaweza kuzinunua mahali popote katika nchi yetu. Ni nini ambalo tunalipendekeza hapa? Katika shule zetu za kufunza elimu ya matibabu ambayo tunaiita Kenya Medical Training College (KMTC) kwa lugha ya kimombo, hilo limewezekana. Hiyo ni kwa sababu yule msichana au mvulana ambaye anasomea KMTC ya Molo, Kitui, Kisumu, Mombasa, Lamu na kila mahali, wako na sare moja. Kama basi inawezekana hivyo kwa mashule yetu ya matibabu, mbona basi isiwezekane kwa mashuleni yetu ya upili na ya msingi katika Jamhuri yetu ya Kenya? Inawezekana! Lakini hapa tukubali ya kwamba halitakuwa jambo rahisi kwa sababu, tukienda kupitisha hili, litakataliwa kwa njia kubwa sana. Tukiongea kule, lazima pia nizungumzie mambo ya vitabu ambavyo vinapelekwa katika shule zetu. Tunasema ya kwamba tunanunua vitabu vyote katika shule haswa za upili, lakini wanaitisha lazima wanunue Bibilia, dikshionari, kamusi na vitabu vinginevyo. Hivyo vitabu pekee yake ni Ksh5,000. Kama tunaweza kununua hivi vitabu vingine vyote, hadi shule zingine ziko na vitabu zaidi, mbona basi tusinunue pia hizi tuweze kuwapa wanafunzi wetu, ili huyu mtoto wa masikini katika nchi yetu ya Kenya awe na nafasi sawa ya kusoma na kufaulu katika maisha kama wa yule wa tajiri? Nakushukuru Mhe. Spika wa Muda."
}