GET /api/v0.1/hansard/entries/1214196/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1214196,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214196/?format=api",
    "text_counter": 34,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Joe Nyutu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Nachukua fursa hii ili niwakaribishe viongozi wa chama cha wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Makueni. Kama wenzangu walivyotangulia kusema hapa Bunge ni mahali ambapo watajifunza mengi kwa sababu sisi hujadiliana kwa amani. Ninatarajia kwamba wakitoka hapa warudi kwenye chuo chao, watakuwa watu wanaoweza kusikiliza wengine, wasimamizi wa chuo na wanafunzi wenzao. Ikiwa kwamba kuna jambo ambalo litakuwa na mukinzano fulani, wanaweza kulisuluhisha kwa kuzungumza kwa amani. Bw. Naibu Spika, sina mengi ila kuwakaribisha huku kama walivyokaribishwa na wenzangu. Niwaambie kwamba Bunge hili ni nzuri na watajifunza mengi ambayo wataenda nayo na wafunze wenzao ambao hawakuja nao leo. Asante, Bw. Naibu Spika."
}