GET /api/v0.1/hansard/entries/1214227/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1214227,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214227/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii kutoa ushauri wangu na kongole kwa viongozi wa Chuo Kikuu cha kutoka sehemu ya Ukambani. Vilevile, naona vipusa wa shule ya upili ambao wamekuja kujionea kwa macho Bunge la Seneti ambalo lina weledi wa kutunga sheria na kuchanganua masuala ya siasa. Pia, kuchanganua masuala ibuka katika nchi ya Kenya. Hii Bunge ambayo ina wazee wengi ambao wana tajiriba ya miaka mingi. Waswahili husema palipo na wazee hapaharibiki neno na palipo vijana chipukizi, wazee hutoa jasho. Hivi kwamba ni kuwaambia viongozi wa vyuo vikuu ambao wako hapa kwamba wao ni kielelezo ama mfumo wa kizazi kipya cha viongozi. Lazima mwelekeze wenzenu kwamba nchi hii haihitaji kutwambia unatoka ukoo upi ama unashiriki dini ipi. Cha muhimu ni kile kilicho kichwani mwako na Mungu unayemwamini. Mwanariadha shupavu, Elid Kipchoge, alisema, mtu hatimiliki, mtu hana kikomo. Cha muhimu ni nia na penye njia. Nyinyi wanafunzi wa vyuo vikuu, mimi wenu vilevile nilikuwa nimejitwika ganzu la kuwa kiongozi katika chuo cha Laikipia kule Nyahururu. Vilevile nilikuwa kiongozi katika shule ya upili niliposoma na bullfighter, Sen. (Dr.) Khalwale. Sasa, tunataraji kwamba yale ambayo yanawakumu nyinyi kama vile kuongezwa kwa karo ya vyuo vikuu, nendeni mjipange, mlete hoja zenu hapa Bungeni, mtueleze mbona hamtaki tuinue gharama ya chuo kikuu na sisi wenu tutawatetea kama wasomi katika Bunge la Seneti. Mimi ni mwalimu wa chuo ya shule ya upili. Nafurahia sana nikiona walimu wenzangu wakileta wanafunzi hapa ili kujionea na kuelewa kwamba hatima yako iko mikononi mwako. Uamuzi utakaochukua kutoka sasa utakuelekeza kule ambako unataka kuwa katika siku za usoni. Bw. Naibu Spika, nashukuru kwa fursa uliyonipa na kuwatakia kila la heri wanafunzi wa vyuo vikuu na wale wa shule ya upili. Mjivunie kuwa Wakenya na katika Bunge la Seneti."
}