GET /api/v0.1/hansard/entries/1214237/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1214237,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214237/?format=api",
"text_counter": 75,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kama mwenyekiti wa Kiswahili kitukuzwe katika Afrika Mashariki na Jangwa la Sahara, ni vizuri nifanyie Kiswahili haki kwa kuwakaribisha wanafuzi wa kutoka shule ya St. Anne Gituba. St. Anne Gituba ni shule moja ya maana sana kutoka Kaunti ya Kirinyaga. Kama mimi niko hapa, pia wao wanaweza kufika hapa. Nimesikia kuwa hapa kuna viongozi wa wanafuzi kutoka chuo kikuu cha Makueni. Mimi sikufanikiwa kuwa kiongozi katika chuo kikuu lakini nilikuwa kiranja katika darasa la saba. Kwa hivyo, nadhani hata huo ni uongozi. Bw. Naibu Spika, nafasi ambayo wanafunzi wako nayo sasa hivi ni muhimu sana. Kuwa na nafasi ya kuja katika Bunge la Seneti kujionea jinsi ambavyo mambo yanafanyika, ni jambo nzuri sana ambalo pia litawasaidia katika maisha yao yajayo. Kwa sasa hatusemi kuwa wao ni viongozi wa kesho, bali wa sasa hivi. Hilo linadhihirika wazi ukiangalia viongozi walio hapa katika hili Bunge la Seneti. Bw. Naibu Spika, ninawakaribisha wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya St. Anne Gituba. Kwa sasa, ningependa kuwakumbusha kwamba kwamba kila kitu kinawezakana."
}