GET /api/v0.1/hansard/entries/1214318/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1214318,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214318/?format=api",
    "text_counter": 156,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, utaelewa kwamba bungeni lazima kuwe na pande mbili ambazo ni kama kueka majembe mawili ndani ya gunia halafu yakose kugongana. Kawaida, lazima yagongane. Kwetu, tukienda shambani tunaweka, tunabeba na kwenda shambani kulima. Kwa hivyo, sisi tukiwa upande huu na wale pande ule, ni lazima kutakuwa na hizo tofauti. Lakini, tumekaa na ndugu yangu, tumeongea na tumekuwa na mwelekeo. Ninakubaliana na yote yaliyosemwa na ndugu yangu, Sen. Cheruiyot. La muhimu ambalo ningependa kukushukuru zaidi ni kwamba wewe kama kinara wetu hapa, umefanya vizuri kutusikiza na nimekwambia maombi yetu. Vile tulivyoafikiana na kukubaliana, nina hakika utayasema hapa. Waswahili wanasema yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Maanake kuna mengi sisi kama viongozi tutapitia na kuyapata. Hii ni safari imeanza. Tuko na wewe kwa miaka mitano na tumeanza tu safari hii. Kwa hivyo, husichoke. Kama sisi ama hao wamefanya chochote hapa, tutajumuika pamoja. Seneti inajulikana kama Bunge ambayo watu wanaelewana na kufanya kazi bila kupendelea upande huu ama ule. Sote tuko sawa. Yale tuliyoyafikiana kwa upande huu, utayasema. Nina imani kwamba utaweza kuwaeleza ndugu zangu kwamba tumesameheana. Hakuna mtu ambaye hawezi kosa kuomba msamaha. Kama tumekukosea---"
}