GET /api/v0.1/hansard/entries/1214387/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1214387,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214387/?format=api",
    "text_counter": 225,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika. Kwanza, ninamshukuru Kiongozi wa Wengi na Kiongozi wa Wachache. Hii ni kwa sababu ninaelewa ya kwamba uchache ya Walio Wachache sio wingi wetu tulio Wengi. Kwa hivyo, ninadhani ni jambo la busara amefanya. Sijui iwapo leo ilikuwa siku yangu katika diary ya shetani. Hii ni kwa sababu, yale mambo yaliyokuwa yanafanyika hapa ndani na hata nje, nimekuwa na matatizo mara mbili. Kwanza, nilikuwa na shule tatu ambazo zimezuru hapa leo. Sijui kwa nini mambo fulani yamefanyika wakati walipokuwa hapa. Iwapo wameenda wakifikiria hivyo ndivyo tunavyofanya hapa, niko na shida kubwa sana."
}