GET /api/v0.1/hansard/entries/1214395/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1214395,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214395/?format=api",
"text_counter": 233,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Chupa za maji ambayo nimekunywa ndizo hizi hapa. Hizi ni nusu tu ya chupa zote za maji niliyokunywa nilipokuwa hapa. Kule nje pia, nimefanya vivyo hivyo. Sasa ninaomba tuweze kwenda mbele kama Bunge ili tutekeleze majukumu yaliyo mbele yetu. Hilo ndilo litatufanya sisi tuonekane kama Maseneta. Kwa bahati mbaya, wote walikuwa wameenda katika Bunge la Kitaifa kisha wakaishia hapa. Sen. Methu na Sen. Joe Nyutu walikuwa wamemalizana na wao. Hata hivyo, kwa sababu diary ya shetani ilikuwepo, ikawa sasa ni zamu ya wale niliokuwa nao. Kuna wengine ambao walikuwa nje na wameenda nyumbani wakiwa wamekasirika sana. Kwa hivyo, twende pamoja. Wakija wakati mwingine, nitampa nafasi Kiongozi wa Wachache ili anitetee. Leo haikuwa siku nzuri lakini pia Mungu yuko katika enzi."
}