GET /api/v0.1/hansard/entries/1214403/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1214403,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214403/?format=api",
"text_counter": 241,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Nitachukua dakika moja tu wala sio mbili. Kwanza, ninatoa shukrani kubwa kuona Kiongozi wa Wengi na wa Wachache, wamekaa chini pamoja na Commissioner Omogeni na kuzungumza ili kupata suluhisho. Kusema kweli, huu ni muhula wangu wa pili katika Bunge la Seneti; Bunge la 12 na sasa hili la 13. Kulikuwa na cheche moto sana katika Bunge la 12 lakini sio kama hii ya leo. Nimeshukuru kuona kwamba kuna viongozi wenye busara katika hili Bunge la Seneti. Wamekaa chini wakaona ni vyema watatue hili swala. Wamekaa chini ili kuweza kutatua jambo hilo. Bw. Naibu Spika, naomba msamaha kwa niaba yao. Uwasamehe ili tuweze kuendelea na kikao chetu kama kawaida kwa sababu kuna mengi ya kuwafanyia wananchi katika kaunti zetu. Sina mengi, Bw. Naibu Spika. Uwe na imani na Bwana asifiwe."
}