GET /api/v0.1/hansard/entries/1214492/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1214492,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214492/?format=api",
"text_counter": 330,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nachukua fursa hii kuunga mkono taarifa iliyoletwa na Sen. Wambua. Ni ukweli kwamba Serikali imechukulia kwa uzito upanzi wa miti. Rais amesema tupande miti. Hili ni jambo la muhimu sana kwa sababu sehemu zilizo na miti kunanyesha lakini sehemu ambazo ni jangwa zimebaki vile kwa sababu hakuna miti. Ninapoongea, ukitembea sehemu ya Laikipia hasa Igwa Miti mahali Laikipia University iko, ni jambo la kuvunja moyo sana, kwa sababu pale kwenye chuo kikuu kazi wanaofanya ni kukata miti usiku na mchana bila kuzingatia yale Sen. Wambua aliyosema kwamba tupande miti. Kamati itakayoshughulikia hili jambo wanafaa washughulikie sio tu sehemu zilizotajwa, washughulikie sehemu za Laikipia hasa Laikipia University kwa sababu hapo ndipo kuna shida kubwa; wanakata miti kiholela na hawapandi. Naunga mkono taarifa iliyotolewa. Ningependa kumueleza Sen. Wambua ambaye ni Naibu wa Kiongozi wa walio Wachache katika Bunge kwamba Serikali ya Kenya Kwanza imejitolea mhanga kupanda miti. Najua hili kwa sababu Waziri anayehusika tumekuwa na yeye Laikipia na tumeamua tutapanda miti. Tayari tuko na miche karibu milioni tatu pale Laikipia. Tunaongoza kutoka mbele na watu wa Kitui wakitaka tutawasaidia na hiyo miche. Asante Bw. Spika wa Muda."
}