GET /api/v0.1/hansard/entries/1214826/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1214826,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214826/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Kuhusu swala la CBC, kwa kweli taifa halijakuwa tayari kwa haya mageuzi ya elimu. Shule zilizochaguliwa kuwa na junior secondary school ni chache ukilinganisha na wanafunzi walio wengi zaidi. Walimu waliochaguliwa ni wachache ukilinganisha na shule na wanafunzi. Fedha, pia, za kuwezesha mchakato huu kuendelea kikamilifu. Shule zote hazina mahabara na CBC haiwezikukamilika bila mahabara. Wazazi wanaumia kifedha kupeleka watoto wao junior secondary schools. Wanaambiwa wabadili sare za shule na pia waende na madawati. Kila siku kuna mambo mapya mpaka inakuwa vigumu kutekeleza swala hili. Kwa hivyo, ninasimama na wengi wa Wajumbe Bungeni ambao wamezungumzia kuwa swala hilo bado; Serikali haijakuwa tayari. Tusizungumze tu bali tutekeleze kwa sababu ya wingi wa waliokataa lisimame. Hatumpingi aliyeanzisha swala hili. Hata mimi namwombea Mhe. Magoha alale pema peponi lakini kwa sasa Serikali haijakuwa tayari na jambo hili. Kila siku mnasikia Serikali ikisema hakuna fedha na kama hakuna fedha wale watoto watasomea wapi? Kila shule inatakiwa iongezwe madarasa na madawati na ukiangalia hazina ya National Government Constituencies Development Fund(NG-CDF) mpaka leo haijatoa hata ndururu ya maendeleo. Ningependa kuungana na wenzangu kupinga hili jambo kuendelea ili turudi katika mfumo wa zamani alafu mbeleni tukiwa tayari tutaweza kuingia. Ningependa kutoa nafasi kwa wenzangu ili waweze pia kupata nafasi ya kuchangia swala hili. Asante sana Mhe. Spika wa Muda."
}