GET /api/v0.1/hansard/entries/1214911/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1214911,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214911/?format=api",
    "text_counter": 330,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante, Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi nichangie jambo hili la masomo ya CBC . Jambo lolote jipya hupata upinzani. Kwa hakika, CBC iko na mapungufu mengi – mapungufu ya upande wa walimu, upande wa wazazi, na kwa majengo kwenye junior secondary school. Tena mapungufu yamezidi kwenye maeneo Bunge mengine. Maeneo Bunge kama Lamu ni visiwa. Hata kama kina wanafunzi wachache, kisiwa ni lazima kiwe na shule na walimu. Ukisema unawatoa wanafunzi kwa kisiwa kizima uwapeleke kwingine, ni shida kwa sababu usafiri ni taabu. Walioanzisha CBC hawakuzifikiria sehemu nyingine. Hatusemi CBC ni mbaya, lakini kuna sehemu haiwezekani. CBC ina uzuri wake. Niko upande wote. Nina mtoto ambaye ako mjini na anasoma CBC . Naona ni mzuri. Lakini kwa ninaowakilisha kule Lamu Mashariki, CBC inawasumbua. Kama alivyosema mwenzangu, inaonekana CBC ni ya matajiri. Uzuri wa CBC ni kwamba mtoto anakua mtoto mzuri aliyefundishwa vyema. Mtoto anakuuliza maswali mpaka wewe kama mzazi wakati mwingine unashindwa kumjibu. Mtoto wangu mdogo ambaye ako darasa la tatu aliniambia anataka kuanzisha biashara. Nikamuuliza anataka kuanzisha biashara gani. Akaniambia anataka kuuza vitabu ambapo kwa wengine ilikuwa haiwezekani. Kwa hivyo, CBC si mbaya. Mheshimiwa Spika wa Muda, hofu yangu kubwa ni kwamba tukifikiria kurudi nyuma kwa sababu kuna shida zaidi, kwenda mbele kutakuwa shida. Sasa, sisi, kama viongozi, tutafute suluhisho mwafaka. Tushirikiane na Wizara ya Elimu, wazazi na walimu ili tuhakikishe mapungufu ya CBC yamerekebishwa. Na ikibidi, kama hatutaki tena CBC, watu wamesema watupe mtoto na maji yake. Tuchunge sana kwa sababu wakati huo pia tunaweza kuleta shida zaidi. Tukibadilisha mtaala huu, tutawapeleka wapi wale watoto wa darasa la kwanza hadi darasa la tatu au nne?"
}