GET /api/v0.1/hansard/entries/1214979/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1214979,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1214979/?format=api",
"text_counter": 54,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ahsante sana, Naibu wa Spika. Kwa niaba ya wananchi wa Igembe Kusini na familia yangu, ningependa kutoa rambirambi kwa familia ya Mhe. Ntoitha M'Mithiaru. Nilijuana na Mhe. Ntoitha M'mithiaru nilipochaguliwa kipindi cha kwanza. Alinionesha vile nafaa kufanya hapa ili nisije nikafukuzwa kazi. Nilifuatilia yale aliyoniambia mpaka nikachaguliwa kwa mara ya pili. Naombea familia yake ili Mungu aendelee kuizingira na damu ya Mwana wake, na Mungu aendelee kuikuza Eneo Bunge hili la Igembe North. Tunamuomba Mungu aiweke roho yake mahali pema anapowaweka watakatifu wake. Amina."
}