GET /api/v0.1/hansard/entries/1215019/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1215019,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215019/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": " Ndio, nitamtambua Mhe. Tandaza. Pia Mhe. Tandaza amevalia vazi la Kiafrika. Asante. Niruhusu niendelee. Bila shaka, hatua hii inaafika hadhi, jukumu, sura na sifa ya Bunge la Kenya. Siku zote jukumu la viongozi ni kupeperusha upekee wa nchi na jamii zao. Kama kielelezo, nimeng’aria vazi lililoshonwa na fundi wangu kule Taita Taveta. Bila shaka, ningeweza kuvaa Uturuki, Uchina, Italia, na mitindo kadha ya ng’ambo. Lakini, viwanda vya Kenya kama Rivatex, Spin Knit Limited na Thika Cloth Mills vitapata riziki yao wapi iwapo kama sisi viongozi hatutachukua hatua ya kwanza? The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}