GET /api/v0.1/hansard/entries/1215020/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1215020,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215020/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta, UDA",
"speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
"speaker": null,
"content": "Kwa juma moja lijalo, kuanzia siku tatu zilizopita, Wabunge wa kike katika Jumba hili na Seneti watavaa mavazi na mitindo ya Kiafrika. Lengo la hamasa hii ni kutangaza mavazi na utamaduni wetu kitaifa na kimataifa. Tunalenga kuinua ufundi wetu na kuboresha mapato ya wanamitindo wetu pamoja na Wakenya wanaofanya kazi katika viwanda vya nguo. Ni sharti tuinue soko la wasanifu na wasanii wetu wa Kenya na Afrika kupitia mavazi, fasihi, teknolojia na sanaa za hapa nyumbani. Nimekuwepo Bungeni humu kwa kipindi kirefu sasa. Bila shaka, nafahamu kuwa Kanuni za Spika zimebainishia Wabunge wa kiume mavazi kama suti, tai na viatu. Kwa hekima yake, Kanuni za Spika zimetuwachia fursa ya kuwa wabunifu katika mavazi ili kuakisi utamaduni na mahitaji ya Bunge na Wakenya. Mavazi kama wanayovaa kaka zangu Wabunge yanahimiza na kuboresha soko la mataifa ya nje ya Afrika. Mavazi ni kitambulisho na sifa ya kila jamii. Mwafrika ni nini kama si chakula, mavazi na lugha zake? Muandishi Shaaban bin Robert alisema titi la mama litamu, hata likiwa la kelbu”. Huu ni utamaduni wetu na ndilo titi la mama yetu. Isitoshe, tasnia ya mavazi na mitindo ni miongoni mwa sekta zinazooajiri Wakenya wengi. Isitoshe, ujasiriamali wa biashara ndogo ndogo kama ya mavazi huchangia mapato yetu na utalii na kubuni ajira na kuleta mapato kwa watu wetu. Mhe. Naibu Spika, tunaomba utuongoze kuungana na wenzetu katika Bunge la Ghana, Bunge la Afrika Kusini, Bunge la Nigeria, miongoni mwa mengine. Wenzetu hao wamekoleza desturi na itikadi ya kuvaa mavazi ya Kiafrika katika Bunge na mikutano ya kimataifa. Mwisho, nahamasisha Wakenya kujivunia mavazi na mitindo ya Kiafrika. Tujiunge na mjadala huu unaoendelea katika mitandao ya kijamii. Nakusihi uruhusu Waheshimiwa Wabunge kutoa na kunakili kauli zao kuhusu suala hili. Hata wewe umevalia vazi la Kiafrika na unapendeza sana. Asante, Mhe. Naibu Spika."
}