GET /api/v0.1/hansard/entries/1215022/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1215022,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215022/?format=api",
    "text_counter": 97,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Migori County, Independent",
    "speaker_title": "Mhe. Fatuma Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Shukran, Mhe. Naibu Spika. Kwanza kabisa, nawashukuru wanaume wetu; wametushangilia wiki nzima. Na mnaonekana kwenye runinga mjichunge nyumbani. Mavazi ya Kiafrika ni kitamaduni kitamu na cha heshima sana. Hata kwa dini na madhehebu tofauti tofauti, mavazi haya yanapendeza. Tukiangazia kabisa mishono hizi tunazozivaa kwa wiki hii yameshonwa na mafundi ambao ni wamama wa hapa nyumbani Kenya. Zaidi ni wamama walioko viungo vya chini. Ni wamama ambao sio wabunifu wa hali ya juu. Kama langu limeshonwa hapa River Road, Nairobi na mama mmoja na ni bei ya chini. Lakini ujue unapomuinua mama moja unainua uchumi ya nchi. Nawaambia wamama tuendelee kuvaa haya mavazi ya Kiafrika. Nama ikiwezekana tukubaliane na hawa wanaume wetu ambao ni mandugu zetu pia wavae vitenge vya kisuti ili waje nayo hapa. Wasiwe wanavaa tu ya kizungu. Hatufanyi kwa sababu tunajiinua; tunawainua wamama walioko chini. Kwa hivyo, fanyeni kwa niaba ya kuhimiza wamama na mafundi ambao ni wamama wa kiwango cha chini na mjue bei itakua chini na itasaidia uchumi ya hii nchi. Hiyo pesa kidogo tunayo tukiwasaidia hao mafundi wetu uchumi yetu itainuka. Naomba wazee waliopo leo wapatie wake wao hela wanunue kitenge. Nawaomba mseme mtafanya hivyo. Mtafanya hivyo? Asante sana."
}