GET /api/v0.1/hansard/entries/1215031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1215031,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215031/?format=api",
"text_counter": 106,
"type": "speech",
"speaker_name": "Busia County, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Catherine Omanyo",
"speaker": null,
"content": " Thank you, Hon. Deputy Speaker. Ninashukuru sana. Nimeambiwa nizungumze kwa Kiswahili. Kuinua uchumi wetu na kuleta pia kazi kwa wamama na wanaume wa kiwango cha chini ni kuwapatia biashara. Kwa hivyo, kuvaa kitenge sio kwa chama pekee yake. Yafaa utamaduni wetu wa Kiafrika tusiusahau kwa sababu tunaiga mifano wa ng’ambo na tunasahau tunaonekana kama puppets . Tunakaa vikaragosi. Unajua ukiomba utamaduni wa mtu mwingine haistiri uchi. Yafaa tusiazimeazime tu kila kitu. Hapa Bunge tuzidi kuwa mstari wa mbele kurudi mahali ambapo tulikotoka. Wazungu ni marafiki wetu lakini ikifika kwa tamaduni zetu, tunafaa kuvaa kama Waafrika, kutabasamu kama Waafrika, kukaa kama Waafrika na kufikiria kiAfrika. Mhe. Naibu Spika, naomba uwe unavaa hivyo kila siku ukiweza. Jinsi umevaa unafanana na malakia ama malkia. Unapendeza sana mpaka nilikuwa nimesahau kama ni wewe. Ujaze kabati na nguo kama hizo kwa sababu heshima inakuja mara moja bila kubembeleza. Nashukuru sana. Nitakuwa navaa kitenge kila siku."
}