GET /api/v0.1/hansard/entries/1215038/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1215038,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215038/?format=api",
    "text_counter": 113,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Westlands, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Tim Wanyonyi",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia fursa ya kuchangia Mswada huu. Kwa niaba yangu, nimefurahi sana kuona Wabunge wetu, akina mama, ambao ni viongozi, wakiongozwa na wewe Mhe. Naibu Spika, wakiingia hapa wakiwa wameng’aa kabisa. Lakini mavazi ni chaguo la mtu. Ila, ningependa kuhimiza akina mama kwamba wakati mwingine mkifanya uamuzi, ni vizuri muungane na wanaume. Mngetuibia hiyo siri, sisi pia tungeweza kuvaa kama nyinyi. Ninafikiria kuwa wakati mwingine huwa mnafanya ubaguzi. Mnafanya mambo pekee yenu kama akina mama halafu mnataka wanaume wawaunge mkono. Ningependa kusema ya kwamba ni jambo la muhimu lakini inafaa mjumuishe kila mtu ndio tujue kwamba hili ni jambo letu sisi sote. Kwa sababu hii ni kimila yetu. Tunataka pia kuona vazi la Kenya kwa sababu haya mavazi mmevaa hapa mengi si ya Kenya. Tunataka kuona lile vazi ambalo limeshonwa na linaitwa Kenya. Hilo ndilo tutafurahia na kuinua kiwango cha wale mafundi, vijana na akina mama wetu ambao wanafanya hii kazi. Serikali ya Kenya Kwanza inatambua hiyo kama “b ottom up”. Hao ndio tunataka kuinua na sisi tutaenda kushona nguo huko. Ni vyema mtuonyeshe mlikoshona nasi pia tuweze kushona shati na vitenge zetu. Asante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi."
}