GET /api/v0.1/hansard/entries/1215040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1215040,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215040/?format=api",
"text_counter": 115,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kamukunji, JP",
"speaker_title": "Hon. Yusuf Hassan",
"speaker": {
"id": 398,
"legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
"slug": "yusuf-hassan-abdi"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia fursa hii. Nachukua nafasi hii kusema kwamba leo ni siku ya furaha na shangwe kwa sababu naona akina mama wetu wamekuwa na mwamko. Wamejitokeza leo kuzatiti na kushikilia kwa nguvu utamaduni wetu wa Kiafrika. Unajua taifa lolote lisilo na utamaduni sio taifa huru. Tumekua na kasumba ya kikoloni ambapo tumeambiwa kuwa mavazi ya kizungu, ndio bora na yenye ustaarabu. Lakini sio hivyo kwa maana Bara la Afrika limekuwa na ustaarabu wa kudumu na wa muda mrefu kwa karne nyingi sana. Ninaona kuwa Bunge hili na akina mama wameonyesha mfano mzuri. Hili ni jambo ambalo litawahimiza akina mama wengine nchini kujua kwamba wana utamaduni na mavazi ya heshima na yenye umaridadi. Nasema hongera sana kwa Bunge hili na kwa akina mama haswa Mbunge wa Taita Taveta, kwa kuleta jambo hili katika Bunge. Na sio jambo la kuomba omba au wanaume wasaidie ila ni wajibu wetu kuunga mkono jambo lolote ambalo linawapeleka mbele akina mama wetu. Jambo hili ni muhimu ili kujionyesha walivyo na kurudi katika utamaduni wao wa kiasili ambao ni wa heshima na mzuri. Kwa hivyo, mimi ninasema kwamba huu ni mwamko ambao utaonyesha mfano mzuri. Hata kwetu wanaume, ninafikiria Bunge libadilishe sheria zake ili tusiwe tunavaa tai kila siku na hizi suti za kizungu. Haina raha! Angalia sasa hivi hali ya hewa ilivyo, ni joto sana lakini unalazimishwa kuvaa tai na koti. Unatokwa na jasho and huna raha kwa sababu ya kasumba ya kizungu. Kwa hivyo, tunahitaji kuwa na ukombozi wa akili na kujifikiria kwa heshima kwamba sisi Waafrika tuna utamaduni na mavazi yetu. Nawapongeza sana na kuwaambia kuwa muendelee kusonga mbele. Nasi wanaume pia tuhimizwe tubadilishe sheria za Bunge ili tuweze kuwa na raha ya kuvaa nguo zetu za kiasili. Huwa ninaona mwenzetu kule Seneti, Seneta wa Narok, akivaa mavazi ya kiasili. Na pia dada yetu huyu kutoka Narok, Mhe. Tonkei, amevaaa za kiasili pia. Wamaasai, Wasamburu na Waturkana wameshikilia utamaduni wao. Hawajatawaliwa kiakili kama Wakenya wengine. Kenya sio kisiwa. Sio lazima tuwe tunaiga kila kitu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}