GET /api/v0.1/hansard/entries/1215148/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1215148,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215148/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "speech",
"speaker_name": "Laikipia North, JP",
"speaker_title": "Hon. Sarah Korere",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": " Kinara wa Waliyo Wachache Bungeni alipozungumza alisema kwa kimombo kwamba wanataka kuchukua hatua za kinidhamu. Utasikiza alivyosema. Mhe. Junet aliposema kuwa wale wanataka kuenda kuchukua nafasi zao katika Kenya Kwanza waende, ninamjulisha kuwa hatuendi. Iwapo wana njia yakutupeleka watafute tingatinga watupeleke. Tutakaa kwenye huu mrengo. Ndugu yetu ambaye ni Kinara wa Wachache hana ule uvumilivu wa kusikiza mawaidha yanayotofautiana na yake. Kwa Kiingereza inaitwa intolerance. Kila mmoja aliye kwenye jumba hili alichaguliwa na alitumia mali zake, akili na hata muda wake kutafuta kura, kujitafutia na kutafutia mrengo wake wa kisiasa. Tusifike hapa watu waanze kuhujumu wenzao kwa sababu wengine wetu wameenda kukutana na Rais wa Kenya. Kuna Rais mmoja Kenya, hakuna mwingine. Kuomba ruhusa ni mamlaka mabaya ya imla, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}