GET /api/v0.1/hansard/entries/1215152/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1215152,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215152/?format=api",
    "text_counter": 227,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia North, JP",
    "speaker_title": "Hon. Sarah Korere",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": " Mheshimiwa Spika ninavyoelewa mimi ni kwamba, kila Mheshimiwa katika Jumba hili ana wajibu wa kuhakikisha kuwa serikali imewajibika. Awe wa upande ule ama upande huu. Ninashangaa kizaazaa ambacho ndugu yetu Kinara wa Waliowachache anataka kuleta kisiri ni cha nini. Iwapo kizaazaa kipo, wasifanye kisiri bali walete kinaga ubaga kwa kuwa chama ninachosimamia… Wajua waswahili husema paka akiondoka panya hutawala. Mhe. Uhuru alipoondoka Jubilee kwa sasa mimi ndiyo Kinara wa chama wa muda. Iwapo wana ODM wanataka mazungumzo basi wazungumze nami. Naomba Kiongozi wa Waliowengi Bungeni alinde uhuru na haki za Wabunge. Ashirikiane na ndugu zetu kwenye Bunge. Waache kwenda Jeevanjee. Waseme kila wanachokitaka wakiwa hapa kwenye Bunge."
}