GET /api/v0.1/hansard/entries/1215332/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1215332,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215332/?format=api",
    "text_counter": 141,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii niweze kuchangia Hoja iliyoletwa mblele ya Seneti. Kwanza kabisa, naiunga mkono kwa sababu ninamjua mhe. Muthama. Pengine ningepata motisha ya kumjua hata zaidi iwapo ningesikia mahojiano na mawaidha yaliyopeanwa hapa na viongozi. Nimewasikia Sen. Cheruiyot, Sen. (Dr.) Khalwale na Sen. Mungatana, MGH, wakisema kwamba walifanya kazi naye kwa muda mrefu. Bw. Spika, mimi nimemjua kama kiongozi wa chama cha UDA na pia mtu mwenye uzoefu sana katika maswala ya kisiasa. Nilipokuwa katika harakati za uchaguzi, nilienda kwake kumuuliza wosia wake kuhusu mambo ya siasa. Nilimuona kama mtu aliyekomaa na kubobea katika kazi yake. Ninasema hivi kwa sababu ukiongea na yeye, anaongea kwa utaratibu huku akijua mambo ambayo anapaswa kulenga. Kwa kuwa amekuwa kiranja wa Walio Wachache na hata wa Walio Wengi katika wakati tofauti tofauti. Kwa hivyo, ninajua ataleta mawiano katika Tume ya Bunge. Kuna viongozi wengi lakini ninajua yeye ni mpole na ana uzoefu wa utendaji kazi. Kwa hivyo, ataleta uongozi mwema katika Tume ya Bunge. Ningependa kufahamisha Bunge hili la Seneti ya kwamba nimezungumza na mhe. Muthama. Maoni yake ni sawa na ya Sen. Cheruiyot ambaye amesema sisi tumekandamizwa kidogo katika Tume ya Bunge. Sitaki kuongea mengi kwa sababu nitamwaga mtama penye kuku wengi. Sisi tayari tunajipanga na tunafanya mambo yatakayoendelea kusaidia Bunge la Seneti. Kwa kuwa mhe. Muthama alihudumu na hatimaye kuacha siasa baada ya kuhudumu katika Bunge la Seneti, ninajua atakuwa mstari wa mbele kutusaidia sisi Maseneta katika kutatua shida tulizo nazo. Ninajua ataangazia kwa mapana na marefu shida nyingi zinazozungumziwa hapa na Maseneta. Bw. Spika, ninaunga mkono na ninamkaribisha katika Tume tufanye kazi pamoja. Ningependa kumhakikishia kwamba tutafanya kazi tukiwa kitu kimoja kwa sababu umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu."
}