GET /api/v0.1/hansard/entries/1215334/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1215334,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215334/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Okenyuri",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Ninaunga mkono Hoja hii ya uteuzi wa mhe. Muthama. Yeye amekuwa na uzoefu wa Bunge na ninajua anajua mahitaji ya Bunge hili. Amefanya kazi kwenye sekta ya biashara, siasa na hata katika chama tawala cha UDA ambapo mimi ni mwanachama. Katika kazi yetu kama vijana tulipokuwa tunashughulika na mambo ya kutafuta kura huku na kule, nilishirikiana naye kwa karibu. Ni mtu ambaye ana roho ya kusaidia hasa vijana. Ni kama baba ambaye anajali masilahi ya watoto wake. Kwa hivyo, uteuzi wake umekuja wakati ufaao. Tunatarajia kuwa atashirikiana na wenzake katika Tume hiyo ili kusaidia Bunge la Seneti. Bw. Spika, jambo la mwisho ni kwamba uzoefu wa mhe. Muthama katika biashara utachangia katika Tume ya Bunge. Sisi kama Wabunge tunaunga mkono uteuzi wake."
}