GET /api/v0.1/hansard/entries/1215667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1215667,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215667/?format=api",
    "text_counter": 95,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": " Ndio, nitamtambua Mhe. Tandaza. Pia Mhe. Tandaza amevalia vazi la Kiafrika. Asante. Niruhusu niendelee. Bila shaka, hatua hii inaafika hadhi, jukumu, sura na sifa ya Bunge la Kenya. Siku zote jukumu la viongozi ni kupeperusha upekee wa nchi na jamii zao. Kama kielelezo, nimeng’aria vazi lililoshonwa na fundi wangu kule Taita Taveta. Bila shaka, ningeweza kuvaa Uturuki, Uchina, Italia, na mitindo kadha ya ng’ambo lakini viwanda vya Kenya kama RIVATEX, Spin- Knit Limited na Thika Cloth Mills vitapata riziki yao wapi iwapo kama sisi viongozi hatutachukua hatua ya kwanza? Kwa juma moja lijalo, kuanzia siku tatu zilizopita, Wabunge wa kike katika Jumba hili na Seneti watavaa mavazi na mitindo ya Kiafrika. Lengo la hamasa hii ni kutangaza mavazi na utamaduni wetu kitaifa na kimataifa. Tunalenga kuinua ufundi wetu na kuboresha mapato ya wanamitindo wetu pamoja na Wakenya wanaofanyakazi katika viwanda vya nguo. Ni sharti The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}