GET /api/v0.1/hansard/entries/1215670/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1215670,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215670/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Migori County, Independent",
"speaker_title": "Mhe. Fatuma Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Shukran, Mhe. Naibu Spika. Kwanza kabisa, nawashukuru wanaume wetu; wametushangilia wiki nzima. Na mnaonekana kwenye runinga mjichunge nyumbani. Mavazi ya Kiafrika ni kitamaduni kitamu na cha heshima sana. Hata kwa dini na madhehebu tofauti tofauti, mavazi haya yanapendeza. Tukiangazia kabisa mishono hii imeshonwa na mafundi ambao ni wamama wa hapa nyumbani Kenya. Zaidi ni wamama walioko viwango vya chini. Ni wamama ambao sio wabunifu wa hali ya juu. Kama vazi langu limeshonwa hapa River Road, Nairobi na mama mmoja kwa bei ya chini. Ujue unapomuinua mama moja unainua uchumi wa nchi. Nawaambia wamama tuendelee kuvaa haya mavazi ya Kiafrika. Naomba ikiwezekana tukubaliane na hawa wanaume wetu ambao ni ndugu zetu pia wavae vitenge vya suti ili waje nayo hapa. Wasiwe wanavaa tu mavazi ya Kizungu. Hatufanyi hivi kwa sababu tunajiinua; tunawainua wamama walioko chini. Kwa hivyo, fanyeni hivyo kwa niaba ya wamama na mafundi ambao ni wamama wa kiwango cha chini na mjue bei ikiwa chini itasaidia uchumi wa nchi hii. Hiyo pesa kidogo tunayo tukiwasaidia hao mafundi wetu uchumi wetu utainuka. Naomba wazee waliopo hapa wawapatie wake wao hela wanunue vitenge. Nawaomba mseme mtafanya hivyo. Mtafanya hivyo? Asante sana."
}