GET /api/v0.1/hansard/entries/1215690/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1215690,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215690/?format=api",
    "text_counter": 118,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Westlands, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Tim Wanyonyi",
    "speaker": null,
    "content": "hapa wakiwa wameng’aa kabisa. Lakini mavazi ni chaguo la mtu. Ila, ningependa kuhimiza akina mama kwamba wakati mwingine mkifanya uamuzi, ni vizuri muungane na wanaume. Mngetuibia hiyo siri, sisi pia tungeweza kuvaa kama nyinyi. Ninafikiria kuwa wakati mwingine huwa mnafanya ubaguzi. Mnafanya mambo peke yenu kama akina mama halafu mnataka wanaume wawaunge mkono. Ningependa kusema ya kwamba ni jambo muhimu lakini inafaa mjumuishe kila mtu ndio tujue kwamba hili ni jambo letu sisi sote. Kwa sababu hii ni mila yetu. Tunataka pia kuona vazi la Kenya kwa sababu haya mavazi mmevaa hapa mengi si ya Kenya. Tunataka kuona lile vazi ambalo limeshonwa na linaitwa Kenya. Hilo ndilo tutafurahia na kuinua kiwango cha wale mafundi, vijana na akina mama wetu ambao wanafanya hii kazi. Serikali ya Kenya Kwanza inatambua hiyo kama “ bottom up”. Hao ndio tunataka kuinua na sisi tutaenda kushona nguo huko. Ni vyema mtuonyeshe mlikoshona nasi pia tuweze kushona shati na vitenge vyetu. Asante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi."
}