GET /api/v0.1/hansard/entries/1215922/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1215922,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215922/?format=api",
    "text_counter": 79,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika. Jambo ambalo linadhihirika wazi katika yale ambayo tunajadili ni kwamba kuna viongozi ama serikali dhalimu ambazo hazifuati sheria. Wananchi wanapoenda kortini na uamuzi kutolewa, viongozi hawa hujitwika mzigo wa kiubabe na kuwafurusha kutoka makaazi yao. Japo serikali ya kaunti inataka kubadilisha sura ya eneo hili, lazima wawe na utu moyoni, kuhusisha wananchi katika mjadala wa kukubali kwamba mradi huo ni muhimu. Kisha, wapeane maeneo mbadala pale ambapo wananchi hao watahamia. Vile vile, wakubaliane na wananchi kwamba wanapohama mahali hapo, mradi utakapokamilika wapewe nafasi ya kwanza kuishi katika maeneo hayo. Ukiangalia katika maeneo kadhaa nchini Kenya wale ambao hufurushwa hawapewi nafasi, na wale ambao wanajenga miradi hii huwa na vikundi vile ambavyo tunaita kwa kimombo “ cartels.” Mradi unapokwisha, watu washagawana vyumba na wakaanza kuishi pale kabla mradi kuisha. Mambo ambayo wameleta katika Bunge yanaendelea hivi sasa katika maeneo mbalimbali ya nchi. Kaunti nyingi zinaweza kufikiira jinsi Serikali ya Kenya Kwanza"
}