GET /api/v0.1/hansard/entries/1215928/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1215928,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215928/?format=api",
    "text_counter": 85,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Nimesikiza hii dua kwa makini na nimesikia malalamishi ya wale waliokuwa wakiongea. Lakini nimeshangaa kwa sababu ninavyomjua Kiranja wetu, yeye ni mtetezi wa walala hoi na wanyonge. Najua Serikali yetu ya Kenya Kwanza imekuja kwa kauli mbiu ya kutetea walala hoi na wanyonge. Huu ndio msimamo wetu dhabiti. Wale watu wa Buxton pale Pwani wako pale kihalali. Ikiwa mzazi wa mtu ameishi pale, mtoto akaishi pale na wajukuu na vitukuu wanaishi pale, kama Serikali inataka kuwajengea nyumba zinazofaa, ni vizuri wenyeji waulizwe. Sheria yetu inasema ni vizuri watu wahusishwe kabla mradi wowote haujatekelezwa."
}