GET /api/v0.1/hansard/entries/1215930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1215930,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215930/?format=api",
    "text_counter": 87,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Sheria yetu inasema uzuri ule unapaswa kuonekana umefanywa. Ni vizuri wenyeji wa Buxton wahusishwe. Sheria zetu za Kenya zinasema watu wapewe nyumba na malezi mazuri. Hii ni jukumu ya Serikali. Kwa hivyo, hawaombi dua kando na maneno ambayo yanasemwa kisheria. Sen. Cherarkey amebobea kwa maswala ya kisheria na namuunga mkono kwa yale amesema. Ni vizuri ile kamati itakayoshughulikia haya mambo iangalie kwa undani. Si suala la Buxton Estate pekee yake kwa sababu kuna watu wengi katika Jamhuri ya Kenya wanaoishi maisha ya kusononeka na uchochole. Itakuwa vyema kama kaamati hiyo itawashughulikia watu wote ambao wanaishi mazingira duni. Sisi sote tuangalie sehemu zote ambazo zimeadhirika. Ukienda mahali panaitwa Marmanet huko kwetu Laikipia, kuna watu ambao walifurushwa makao yao na sasa wanaishi barabarani, mahali ambapo hakuna choo wala shule. Ukiwaangalia unashindwa kama wanaishi katika Jamhuri ya Kenya. Kamati isiangalie Buxton Estate pekee yake. Wanafaa watembelee sehemu zingine kama kule Laikipia, Rumuruti, Majengo huko Nanyuki mpaka Maina Village. Hawa watu wote ni Wakenya na ni jukumu ya Serikali kuwalinda na kuimarisha maisha ya wananchi wote wa Kenya. Bw. Spika, naunga mkono dua hii."
}