GET /api/v0.1/hansard/entries/1215932/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1215932,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215932/?format=api",
    "text_counter": 89,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kibwana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 277,
        "legal_name": "Kibwana Kivutha",
        "slug": "kibwana-kivutha"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Pia mimi naunga mkono hii dua. Nazungumza nikiwa na uchungu sana kwa sababu Buxton ni nyumbani. Nyanya yangu ameishi hapo zaidi ya miaka 50 na ametolewa--- Nikizungumzia hili jambo napatwa na emotions. Samahani kwa kuchanganyisha lugha. Watu wa Buxton Estate wameumia sana. Wote walifurushwa na chochote walichopewa kilikua duni sana cha kuwapa nafasi ya kupata mahali pengine pazuri pa kuishi. Ni lazima waangaliwe na wasaidiwe ili wapate nafasi nzuri kuishi vile walikuwa wanaishi kitambo. Bw. Spika, nyumba zenyewe zilikuwa zimedhoofika na kuna watu walitumia pesa nyingi kujaribu kutengeza nyumba zao. Wakati walipokuwa wanaondolewa walikuwa washatengeneza hizo nyumba na hawakulipwa. Zile pesa walipewa hazikutosha kile kiwango walikua wametumia. Buxton Estate ni nyumbani. Ndugu zangu wengine wamezaliwa hapo. Naomba Wakenya waunge mkono dua hii, ili watu wa Buxton wapewe nafasi yao na hadhi zao. Watu wengi huko walikuwa wanafanya kazi na wakastaafu wakiwa huko. Walikaa hapo wakiwa vijana mpaka wakastaafu. Inafaa washughulikiwe ili waishi kama watu wengine nchini. Naunga mkono, Bw. Spika."
}