GET /api/v0.1/hansard/entries/1216098/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1216098,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1216098/?format=api",
    "text_counter": 255,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "mtu binafsi. Katika Kenya, hakuna maji, chakula na hata samaki wanahangaika. Watoto wetu hawana pesa za kwenda shule na vitu vyote vimezoroteka. Kwa wiki mbili au tatu zilizopita tumeshangazwa sana na vitendo vya Maseneta wa upande wa walio wachache. Hii sio mambo ya vyama. Ni mambo ya kuongezea kaunti hela ndio watoto wetu waweze kuenda shule, tupate maji na hospitali zetu ziwe na madawa. Bi. Spika wa Muda, tuko na Serikali yetu ya Kenya Kwanza ambayo inafanya kazi kuliko Serikali zile zingine halafu watu wengine wanatoroka. Ningeuliza kama inawezekana tuseme hii hoja imepita. Hapa hakuna mambo ya mtu binafsi wala vyama, ni mambo ya kushughulikia kaunti zetu kwa kipindi hiki cha miaka mitano. Naunga mkono mjadala huu ili tuweze kuona vile kutakua. Ni mambo ya ajabu wao kusema ya kwamba wanaenda kwa mawe. Ningependa kuwaambia kwamba mambo ya mkate nusu au tosti hakuna. Asante."
}