GET /api/v0.1/hansard/entries/1216162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1216162,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1216162/?format=api",
"text_counter": 319,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Ni kinaya sana sasa vikosi vyetu vimevaa mavazi ya kivita kule Congo na Somalia, na huku kwetu vijijini Wakenya wanamlilia Mungu wakiuliza ni makosa gani walifanya? Tumeona viongozi wakipaa kwenye ndege na magari ya kifahari yakitua na kuenea maeno haya ya vita lakini mpaka sasa hatujaona hatua yoyote ikichukuliwa. Mimi husema “mzaha mzaha utunuka usaa”. Haya ambayo wanafanya sasa wakitarajia kwamba ni ozoefu, yatakuja kuenea maeneo mengine nchini Kenya na watu wataanza kujipanga kisirisiri. Naomba Serikali iwache kufanya mchezo, iende katika maeneo haya ipambane na hao watu. Itakuaje tuko na idara ya ujasusi Kenya hii ambayo vile vile tuanaambiwa ina uzoefu mkubwa; itakuwaje hawajui hawa watu hufanya mazoezi wapi na silaha hizi zinatoka wapi? Itakuwaje shule inatekwa nyara na kila kijiji kina nyumba kumi, naibu wa chifu na chifu na huku tunakuja kusikiza haya mambo kwenye Seneti? Nadhani kwamba kuna biashara ambayo watu wanafanya humu Kenya na nchi za kigeni. Wanatumia vita hivi kupata mishahara ilhali watu wanakufa na wanaenda kungoja hukumu mbinguni kabla wakati wao hujafika. Naomba Serikali, kwa niaba ya maeneo ambayo Wakenya wanavumilia kuwa Wakenya, tuwache kujiongelesha kwenye vyombo vya habari. Tunataka kuona vitendo, ukombozi, uhuru wa Wakenya wajivunie kuishi Kenya. Naomba kwamba idara hizi zote zilete ripoti hapa. Idara ya Ujasusi na Usalama inafaa ikuje hapa watueleze shida iko wapi. Haya maeneo lazima yawe na vijana na wasichana ambao wako katika Idara ya Ujasusi ili waweze kutuambia mambo yanayo endelea huko. Haiwezekani tangu Uhuru bado tunakuja kulilia hapa Bunge tukijiuliza maswali namna hii. Naomba Serikali yangu ya Kenya Kwanza tuamke na tufanye kazi. Asante."
}